Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2016

Ronaldo amkunjia sura Zidane wakati akipumzishwa

Cristiano Ronaldo ameonesha kitendo cha utovu wa nidhamu mbele ya kocha wake Zinedine Zidane pale alipofanya uamuzi wa kumpumzisha mshindi huyo wa Champions League na European Championship wakati wa game dhidi ya Las Palmas. Ronaldo alikunja sura kuonesha kuchukizwa na maamuzi ya Zidane kuhusu kumpumzisha. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kupumzishwa kwa sababu za kiufundi wakati wa mchezo mgumu. Wakati Ronaldo anapumzishwa dakika ya 72, Real Madrid ilikuwa inaongoza kwa 2-1 mbele ya Las Palmas. Zikiwa zimesalia dakika 5 mechi kumalizika, Las Palmas wakasawazisha kwa goli la Sergio Araujo. Mwisho wa mchezo, Real Madrid ikapoteza pointi mbili wakati ilikuwa ikipambana kurejea kileleni mwa La Liga baada ya Barcelona kushinda 5-0 kwenye mechi yao ya mchana.

Kamati ya katiba, sheria kujadili kesi 13 pamoja na ya mchezaji Hassan Kessy

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji leo Jumamosi Septemba 24, 2016 itasikiliza mashauri 13. Malalamiko hayo ni: 1.Mchezaji Ametre Richard ambaye atawasilisha mbele ya kamati makubaliano waliyokubaliana kukaa pamoja na kufikia mafaka. 2. Klabu ya Coastal Union dhidi ya Simba kuhusu madai ya fidia kwa wachezaji Hamad Juma na Abdi Banda. 3. Ally Rashid Ally dhidi ya Simba, malalamiko ya kunyimwa stahiki zake 4. Mchezaji Abdallah Juma dhidi ya Mbeya City, madai ya malimbikizo ya mshahara, fedha za usajili na gharama za matibabu. 5. Simba dhidi ya Young Africans, madai ni kuingia mkataba na mchezaji Hassan Kessy wakati ana mkataba na Klabu ya Simba 6. Kocha Abdul H. Banyai, kesi ni madai ya stahiki zake. 7. Coastal dhidi ya Young Africans, madai ya fidia ya matunzo ya mchezaji Juma Mahadhi 8. Saleh Malande dhidi ya Ndanda FC madai ya uvunjikaji wa mkataba 9. Coastal Union dhidi ya Mbeya City, madai ya fidia ya fidia kwa matunzo ya mchaji wao. 10. Sp

Tazama muonekano wa ndani wa jengo jipya la j.k. Nyerere airport terminal iii jijini da

  Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam ambalo bado linaendelea na Ujenzi.   Mafundi wakiendelea na kazi ndani ya jengo (terminal 3).

Ajibu, Mavugo, waendelea kuchafua rekodi ya Mtibwa mbele ya mnyama

Magoli ya Ibrahim Ajibu na Laudit Mavugo yametosha kufanya Simba iendeleze ubabe mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kuifunga kwa mara nyingine tena kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Magoli yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha pili baada ya timu hizo kutoka sare katika dakika 45 za kipindi cha kwanza. Mchezo huo uliwafanya Mzamiru Yassin nw Shiza Kichuya kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mara ya kwanza tangu wasajliwe Simba msimu huu wa dirisha la usajili. Ibrahim Mohamed ni mchezaji mwingine ambaye alisajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa lakini hakupata nafasi ya kucheza. Dondoo kwa namba 30 Namba kubwa zaidi ya jezi ilivaliwa na golikipa wa Mtibwa Sugar. 10 Pointi ambazo Simba imefikisha baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa. 6 Pointi za Mtibwa baada ya kucheza mechi nne. Imeshinda mechi mbili na kupoteza michezo miwili. Katika mechi saba zilizopita, Mtibwa haijapata ushindi ushindi dhidi ya Simba. Imetoka sare kwenye mechi mb

yanga sc yazinduka

YANGA SC imezinduka katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Maji Maji ya Songea mabao 3-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Amissi Joselyn Tambwe alifunga mabao mawili kipindi cha pili baada ya kiungo Deus David Kaseke kutangulia kufunga kipindi cha kwanza. Yanga sasa inafikisha pointi saba, baada ya kucheza mecni tatu, ikishinda mbili na sare moja – sawa na mahasimu wao, Simba SC. Winga Simon Msuva hakuwa mwenye bahati leo, baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao, ikiwemo penalti.  Msuva alipiga penalti mbili zote akafunga, lakini refa akamuamuru kurudia, ya kwanza akidaiwa kutishia kabla ya kupiga na ya pili, refa akisema wachezaji wenzake walisogea kabla hajapiga. Msuva alipokwenda kupiga kwa mara yatatu, mpira ukagonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya kutokea piga nikupige na kumkuta Kaseka aliyefunga dakika ya 19. Tambwe akaifungia Yanga bao la pili kwa kichwa akimalizia pasi ya

Facebook yarejesha picha ya 'msichana wa Napalm'

AFTENPOSTEN/NICK UT   Espen Egil Hansen ni mhariri wa gazeti la Aftenposten, Gazeti maarufu zaidi nchini Norway Facebook imebatilisha uamuzi wake wa awali wa kufuta moja ya picha mashuhuri ya wakati wa vita vya Vietnam. Picha hiyo inamuonyesha mtoto msichana aliyekuwa bila nguo akikimbia moto katika kijiji kimoja, katika shambulizi lililotekelezwa kwa kutumia kemikali ya napalm. Facebook ilifuta picha hiyo kwa misingi kwamba ilikuwa ya uchi. Facebook inasema imerejesha picha hiyo kutokana na umuhimu wake wa kihistoria. Gazeti moja nchini Norway, Aftenposten, liliongoza shutuma dhidi ya Facebook, baada ya kampuni hiyo kufunga akaunti ya mmoja wa wanahabari wake, aliyetumia picha hiyo. Mhariri wa gazeti la Afte-posten la Norway, amesema uamuzi wa Facebook kufuta picha hiyo inaonyesha wazi haiwezi kutofautisha kati ya picha za ponografia na zile zinazohusiana na historia ya matukio

Gondwe akamata malori usiku

Handeni. Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amekamata malori saba yakisafirisha madini ya chuma aina  dolomite yanayotumika kutengeneza saruji. Gondwe amesema kati ya  malori saba walifanikiwa kukamata matano, huku mawili madereva wakiwahi kutoroka. “Malori hayo yalikuwa yanatokea Kata ya Mgambo, yanakochimbwa madini hayo,” amesema. Kufuatia hatua hiyo, Gondwe ametangaza kupiga marufuku usafirishaji  madini usiku. “Tulipokamata magari hayo, kwanza tuliwauliza kama wamelipa kodi na kama wamelipa watuonyeshe stakabadhi,” amesema. Alisema madini yanapo safirishwa nje ya wilaya mfanyabiashara anatakiwa kuilipa Serikali Kuu asilimia tatu na halmashauri inatakiwa kulipwa asilimia 0.3 ya mauzo. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, William Makufwe amesema wamekuwa wakipoteza mapato kupitia wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi. Makufwe amesema  wameanza kukusanya  kodi  kwa kutumia wataalamu wao na kuachana na mawakala, ambao walikuwa wana

Ummy Mwalimu: Marufuku Kuozesha Waliomaliza La 7

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. SERIKALI imewaonya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutowaozesha watoto wote wa kike waliohitimu darasa la saba mwaka huu wakati wa kipindi hiki cha kusubiri matokeo yao, iwe ni kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya mahari. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mkono wa serikali kisheria ni mrefu, hivyo wazazi au walezi watakaokwenda kinyume watahakikisha kuwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani. Ummy ameyasema hayo jana katika tamko maalumu alilolitoa kwa wanafunzi hao waliohitimu elimu ya msingi nchini kote. Alisema wazazi na walezi wanapaswa kutambua umuhimu wa mtoto wake kuendelea kielimu, na kukua kimwili na kiakili kabla ya kuingia katika ndoa kwani elimu ya watoto wa kike ni moja ya njia bora za kupunguza umaskini katika mataifa yanayostawi. “Natoa rai kwa wananchi wote kuendelea kutoa taarifa kwa mamlak

Waislamu waanza Hija Saudi Arabia

  Usalama mkali umedumishwa nchini Saudi Arabia Takriban Mahujaji wa kiislamu milioni 1.5 wamekusanyika nchini Saudi Arabia chini ya ulinzi mkali, kabla ya kuanza rasmi ibada ya hija ya kila mwaka. Magari yamepigwa marufuku ya kukaribia msikiti mkuu, Grand Mosque, ambao ni eneo takatifu zaidi kwa waislamu, huku mahujaji wakifanyiwa ukaguzi na polisi katika vituo kadhaa kwenye eneo hilo.  Hija hii ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kidini duniani Zaidi ya mahujaji 2000 waliaga dunia mwaka jana wakati wa ibada ya hija, wengi wao wakiwa raia wa Iran. Iran iliilaumu Saudi Arabia kwa kutosimamia ibada za Hija inavyofaa, na imekataa kuwaruhusu raia wake kuenda Saudi Arabia kuadhimisha ibada ya Hija. Hija hii ni ya kuimarisha undugu katika dini ya kiislamu

Abbas ‘Barthez’ Pira: Mlinda Mlango wa Tanzania aliyepo kwenye majaribio Chelsea FC (Picha)

  Panapo majaaliwa, Tanzania inaweza ikawa na mchezaji atakayepiga na klabu ya Chelsea ya Uingereza. Abbas ‘Barthez’ Pira akiwa kwenye majaribio Stanford Bridge Abbas ‘Barthez’ Pira amechukuliwa kufanyiwa majaribio na klabu ya Chelsea inayomilikiwa na bilionea wa Urusi, Roman Abramovich. Barthez akisikiliza maelekezo ya kocha Pira ni mlinda mlango aliyewahi kuichea Coastal Union ya Tanga. Kutokana na uwezo wake katika kupangua mashuti anapokuwa golini, mchezaji huyo kijana aliitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kikijiandaa na kuchuana na Chad kwenye mchezo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) kabla ya Chad kujitoa. Na mwezi huu, Septemba, Pira ameanza taratibu kuiishi ndoto yake ya muda mrefu – kuchezea Chelsea. “Finally made it to Chelsea FC trialist. Proud to be a first Tanzanian to go on Trial at Chelsea FC,” ameandika kwenye Twitter. Tazama picha zake zaidi.

Magufuli aipa makali NHC

Rais John Magufuli .  Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa wizara zote zinazodaiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ziwe zimelipa madeni yao na zikishindwa ziondolewe kama ilivyokuwa kwa kampuni ya Mbowe Hotels inayomilikiwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Rais pia amefanyiwa maombi maalumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Paul Makonda alipotembelea Chuo Kikuu (UDSM), ambako mkuu huyo wa mkoa alisema katika maombi yake kuwa Magufuli ndiye ambaye wananchi walimtaka na kumuomba Mungu azidi kumsaidia katika kutekeleza majukumu yake. Katika shughuli ya awali, Rais Magufuli alitoa maagizo kwa taasisi hizo alipozungumza na wananchi wa Magomeni wilayani Kinondoni kwenye eneo la Magomeni Quarters ambako Manispaa ya Kinondoni ilibomoa nyumba za wakazi miaka mitano iliyopita kupisha ujenzi wa nyumba za kisasa, ikiahidi kuwalipa wananchi hao kodi ya mwaka mmoja na kuwarejesha baada ya ujenzi kukamilika. Hata hivyo, manispaa hiyo imeshindwa

Wanafunzi 3918 wachaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa awamu ya pili

WANAFUNZI 3,918 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kujaza nafasi zilizokuwa wazi kutokana na ufinyu wa nafasi na baadhi ya wanafunzi kutoripoti kwa wakati. Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe ilisema kati ya wanafunzi hao wasichana ni 2,413 na wavulana 1,505. “Kuchaguliwa kwa wanafunzi hao kumefuatia kuwapo kwa nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni tangu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika awamu ya kwanza” alisema Mhandisi Iyombe. Aidha Mhandisi Iyombe alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 1,864 sawa na asilimia 47.58 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo kati yao   wasichana 1,099 na wavulana 765. Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa katika masomo ya Sanaa na Biashara wanafunzi takribani 2,054 (52.42%) wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo, ambapo kati yao wasichana ni 1,314 na wavulana 740. “Wana

Yanga,Ndanda zatambiana

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Hans Pluijm na mwenzake, Hamimu Mawazo wa Ndanda kila moja ametamba kupata ushindi katika mchezo utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. Mabingwa watetezi, Yanga wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mchezo mmoja, lakini ikiwa na michezo miwili mkononi dhidi ya Ndanda kesho, kisha Jumamosi itacheza na Majimaji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pluijm amesema wanatakiwa kushinda michezo hiyo ili wakae sawa kiakili kwani kushinda mechi moja pekee bado hawawezi kujisifu ukizingatia wao ndiyo mabingwa watetezi. “Tunaendelea na maandalzi kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Ndanda, tunatakiwa kushinda ili kujiweka sawa katika ligi. “Tutakuwa na kazi kubwa msimu huu kutetea ubingwa kwani kila timu inatutolea macho na tunakamiwa kwa sababu kila mpinzani wako anataka pointi dhidi yako. “Licha ya kwamba hatujapumzika tangu kumalizika kwa ligi ya msimu uliopita n

SV98 yabadili jina la uwanja kumuenzi shabiki wake

 Klabu ya soka inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) SV Darmstadt 98 imetangaza kubadili jina la uwanja wa klabu hiyo na 'Jonathan Heimes' ambalo ni jina la shabiki wa klabu hiyo aliyefariki mwezi Machi mwaka huu. Taarifa ya Klabu hiyo imesema Jonathan Heimes enzi za uhai wake alichangisha maelfu ya Euro kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Saratani ambapo shabiki huyo alikufa kwa ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 26. Uwanja huo ambayo unajulikana kwa jina la The Merck-Stadion am Boellenfalltor sasa utatambulika kwa jina la Jonathan-Heimes Stadion am Boellenfalltor kwa kipindi cha mwaka mmoja msimu wa 2016-17. Nahodha wa klabu hiyo Aytac Sulu amekaririwa akisema kwamba "kila anayejitambulisha nasi anajitambulisha na Jonathan,". Naye mzazi wa Heimes Martin amesema klabu hiyo na wadhamini wake wameonesha tendo kuu.

Aliyefanyiwa upandikizaji wa kwanza wa uso afariki

Madaktari nchini Ufaransa wamefichua kwamba mwanamke aliyefanyiwa upasuaji wa kwanza wa upandikizaji wa sura alifariki mapema mwaka huu. Hospitali moja imesema kuwa Isabelle Dinoire alifariki baada ya matatizo yanayohusishwa na upasuaji huo . Alifanyiwa upasuaji huo uliochukua saa 15 mwaka 2005 baada ya kujeruhiwa na mbwa. Madaktari waliutengeza mdomo wake,pua na taya katika upasuaji huo wa kwanza kuwahi kufanyika. Hospitali hiyo imesema kuwa kifo chake hakikutangazwa hadi sasa ili kulinda faragha ya familia yake. Alikuwa na umri wa miaka 49.

NDANDA VS YANGA – KULINDA REKODI VS KUVUNJA REKODI

Ligi kuu Tanzania bara itaendelea tena Jumatano ya September 7 kwa mechi tatu kuchezwa kwenye viwanja tofauti, game ya Ndanda FC vs Yanga ni miongoni mwa mechi kali inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa soka kutokana na rekodi zilizopo kati ya timu hizi mbili tangu zimeanza kukutana kwenye ligi baada ya Ndanda kupanda daraja miaka ya hivi karibuni. Ndanda watakuwa wenyeji wa mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara kusini mwa Tanzania. Inatabiriwa mechi hii kuwa ngumu kwa kila upande, ugumu unaosababishwa na matokeo ya timu hizi tangu zilipoanza kukutana. Kila timu itataka kutengeneza rekodi yake, Ndanda wakitaka kutunza rekodi ya kutopoteza mchezo dhidi ya Yanga wakiwa nyumbani wakati Yanga wao wakitaka kuvunja mwiko kwa kuifunga Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona. Mechi zilizopita 2016-2017 Ndanda imeshacheza mechi mbili na kupoteza mechi zote ambapo imecheza nje ya uwanja wake. Ilifungwa 3-1 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa ufu

Sheria ya Vyombo vya Habari kukamilika mwaka huu

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari utafikishwa bungeni mwaka huu wa fedha na sheria yake itakamilika ndani ya kipindi cha mwaka huu. Nape aliyasema hayo wakati akizungumzia utekelezaji wa mipango na mikakati ya wizara yake katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). “Tunatarajia kwamba Bunge hili linaloanza Septemba 6 (leo), tunaweza kuupeleka Muswada huu bungeni ukasomwa kwa mara ya kwanza, na Bunge la Novemba tukaanza mjadala wake na nina matumaini kwamba huu mwaka wa fedha hautaisha kabla hatujapitisha muswada huo,” alisema. Alisema; “Muswada umefikia mahali pazuri na tumeukamilisha sasa tupo tayari kufuata taratibu za kawaida za kuufikisha bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza na ni muswada ambao ni mzuri, utaondoa kelele nyingi ambazo zimekuwa zikizungumzwa, tumekuwa na Sheria tangu mwaka 1976 ambazo zimekuwa zikilalamikiwa.” Alisema

Watoa taarifa feki za uhalifu kutupwa jela

WIZARA ya Katiba na Sheria imesema watakaobainika kutoa siri za watu wanaotoa taarifa za uhalifu na wale ambao watabainika kutoa taarifa za uongo za uhalifu, watatozwa faini ya Sh milioni tatu au kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Utekelezaji wa Katiba, Kamana Stanley alisema kumekuwepo na watu wanaovujisha siri za watoa taarifa na mashahidi wa matukio ya uhalifu, kitendo ambacho kinasababisha watu hao kupata madhara na kuingiwa na hofu ya kuendelea kutoa taarifa. Alisema kuwepo kwa Sheria ya Kuwalinda Watoa Taarifa za Uhalifu na Mashahidi ya mwaka 2017, iliyoanza kutumika rasmi Julai Mosi mwaka huu, itasaidia kuwapatia ulinzi wa kisheria wale wote wanaotoa taarifa za uhalifu wa makosa mbalimbali wanayoyashuhudia yakitekelezwa. “Kumekuwa na woga kwa wale walikuwa wakitoa taarifa lakini tunaamini kupitia sheria hii kutawafanya wao kuwa huru na kuleta matokeo chanya

Ukawa sasa kurejea bungeni

Dar/Mikoani. Baada ya siku 32 za kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika Tulia Ackson, wabunge kutoka vyama vinavyounda Ukawa wameamua kurejea bungeni na kiongozi wao amesema mapambano ya kupinga ukandamizwaji na matumizi mabaya ya madaraka yatahamia kwenye chombo hicho. Wabunge hao wamesema uamuzi wao unatokana na kutii wito wa viongozi wa dini na hekima za Spika Job Ndugai aliyeonyesha utayari wa kushughulikia madai yao. Katika mkutano wa Bunge la Bajeti lililohitimishwa Juni 30, wabunge wa Ukawa, inayoundwa na vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, NLD na CUF walikuwa wakitoka ukumbini kila wakati Dk Tulia alipoongoza vikao, wakidai kuwa hawama imani naye kwa kuwa anawabagua na kukandamiza demokrasia ndani ya chombo hicho. Na kutokana na Spika Ndugai kuwa nchini India ambako alikwenda kuchunguzwa afya yake, Dk Tulia ameongoza karibu vikao vyote vya nyakati za asubuhi na jioni na hivyo wabunge hao wa upinzani kuwa wanaingia ukumbini asubuhi na baada ya sal

Picha: Kiatu maalum cha Adidas atakachovaa Pogba katika mechi na Man City

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas imeonyesha kiatu maalum mchezaji wa Man Utd Paul Pogba kwenye mechi yao na Man City Derby wekeend hii. Adidas wamemtengenezea Paul Pogba viatu maalum ambavyo atavitumia siku ya mechi yao na Manchester City. Adidas ndio wanamdhamini mavazi ya michezo mchezaji Paul Pogba wametengeneza kiatu maalum kwa ajili ni mchezaji wao. Kiatu hichi ni “Adidas ACE16 + Purecontrol Viper Pack”.

Ofisi ya makamu wa Rais yapinga taarifa za kujiuzulu kwa Mama Samia Suluhu

Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni ambazo zinazodai kuwa makamu huyo wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameomba kujiuzulu nafasi yake hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo, habari hizo zilizoenezwa mitandaoni ni za uzushi na uongo kwa kuwa zinalenga kuleta uchochezi na kuliweka taifa kwenye taharuki. Taarifa ya ofisi hiyo imeendelea kwa kuwataka wananchi wote kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya viongozi hao wa serikali ya awamu ya tano. Wakati huo huo ofisi hiyo imewataka watanzania wote kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Mifuko ya hifadhi ya jamii kujenga viwanda vitakavyoajiri asilimia 40 ya Watanzania

Shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania (TSSA) limeazimia kujenga viwanda vitakavyoajiri zaidi ya asilimia 40 ya watanzania na limeitaka serikali kuboresha mitaala kwenye vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili kupata wataalam watakaovihudumia. Shirikisho hilo limesema litajenga viwanda vikubwa, vya kati na vidogo vitakavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini ili kupanua wigo wa ajira kwa watanzania. Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Meshack Bandawe amesema baadhi ya viwanda hivyo vitajengwa na mashirika hayo na vingine vitajengwa na shirika moja moja kulingana na maeneo na upatikanaji wa rasilimali na kipaumbele kitatolewa kwa viwanda vya nguo, sukari, vipuri, chai na madawa. Kabla ya shirikisho hilo kutangaza azma hiyo ya kujenga viwanda, shirikisho hilo lilikutana na mawaziri wa wizara za viwanda, biashara na uwekezaji,kilimo,mifugo na uvuvi, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge,vijana, ajira na walemavu, afya na maendeleo y

TFF watuma salamu za shukrani kwa Gavana wa Nigeria kwa kuizawadia Taifa Stars dola 10,000 za Marekan

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za shukrani kwa Gavana wa Jimbo la Akwa Ibom, Gabriel Emmanuel kwa zawadi ya dola 10,000 za Marekani (sawa na Sh milioni 21.5) kwa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ baada ya kuonesha mchezo mzuri na wa upinzani dhidi ya wenyeji Super Eagles ya Nigeria uliofanyika Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo. Taifa Stars ilicheza mechi hiyo Jumamosi Septemba 3, 2016 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017). Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Taifa Stars ilifungwa bao 1-0 mara baada ya kuibana Super Eagles hivyo kumsukuma Gavana huyo kuandaa hafla ya chakula cha jioni ambako mbali ya kuizawadia Stars, pia aliizawadia Super Eagles dola 35,000 za Marekani. Taifa Stars ilitua Dar es Salaam usiku wa kuamkiia leo Septemba 5, 2016 ambako baadhi ya wachezaji walipelekwa Hoteli ya Urban Rose, iliyoko

Mwasiti kufungua NGO ya mambo ya elimu

Msanii mkongwe wa muziki Mwasiti Almas ameweka wazi mpango wake wa kufungua NGO ambayo itakuwa inasaidia vijana wa kike katika ya elimu. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Unaniangalia’ amesema baada ya kufanya kazi ‘Sister Tanzania’ ameona vijana wengi wanakosa elimu kutokana na changamoto mbalimbali. “Ili kudhibitisha kwamba napenda kujitolea kwa jamii katika siku za hivi karibuni natarajia kufungua NGO ya mambo ya elimu na ninaamini nitaifikia namba kubwa ya vijana wa Tanzania,” Mwasiti aliliambia gazeti la Mtanzania. “Lengo langu ni kuwatoa vijana sehemu moja na kuwapeleka nyingine kupitia elimu itakayokuwa naitoa maana wapo watu wanatamani kufika mahali nilipo lakini hawajui namna ya kufika… hii haitakuwa mara yangu ya kwanza kwa sababu nimefanya kazi na Sister Tanzania na nimepata uzoefu wa kutosha. Mfano kuna mambo ambayo kama msanii nikimwambia mtoto inakuwa rahisi kutekeleza kuliko akiambiwa na wazazi wake.”