Ruka hadi kwenye maudhui makuu

yanga sc yazinduka

YANGA SC imezinduka katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa Maji Maji ya Songea mabao 3-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es SalaamImage result for yanga vs majimaji

Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Amissi Joselyn Tambwe alifunga mabao mawili kipindi cha pili baada ya kiungo Deus David Kaseke kutangulia kufunga kipindi cha kwanza.
Yanga sasa inafikisha pointi saba, baada ya kucheza mecni tatu, ikishinda mbili na sare moja – sawa na mahasimu wao, Simba SC.
Winga Simon Msuva hakuwa mwenye bahati leo, baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao, ikiwemo penalti. 
Msuva alipiga penalti mbili zote akafunga, lakini refa akamuamuru kurudia, ya kwanza akidaiwa kutishia kabla ya kupiga na ya pili, refa akisema wachezaji wenzake walisogea kabla hajapiga.Msuva alipokwenda kupiga kwa mara yatatu, mpira ukagonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya kutokea piga nikupige na kumkuta Kaseka aliyefunga dakika ya 19.
Tambwe akaifungia Yanga bao la pili kwa kichwa akimalizia pasi ya Simon Msuva kufuatia krosi ya Juma Mahadhi. Tambwe akafunga bao la tatu akimalizia krosi ya Mahadhi tena.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imelazimishwa sare ya 2-2 na ndugu zao Stand United Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mbeya City imefungwa nyumbani 2-1 na Azam FC na Ndanda FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar, Ruvu Shooting imewalza ndugu zao JKT Ruvu 1-0 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani. 
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Vincent Andrew/Kevin Yondan dk85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Yussuf Mhilu dk88, Obrey Chirwa/Juma Mahadhi dk46, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke. 
Maji Maji: Agathon Anthony, Bahati Yussuf, Suleiman Kibuta, Hamad Kibopile, Ernest Raphael, Lulanga Mapunda, Alex Kondo, Mfanyeje Yusuph, Hassan Hamisi, Marcel Bonivanture na Paul Mahona/Peter Mapunda dk55.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMA BIBLIA TAKATIFU HAPA

                                                        BONYEZA HAPA KUSOMA BIBLIA       

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO.

 Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na  Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.  Profesa Saber  M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo leo.   Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa.  Kutoka kushoto ni

UNGANA NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE KATIKA KUABUDU.UNGANA NAE UBARIKIWE.