Magoli yote ya Simba yamefungwa katika kipindi cha pili baada ya timu hizo kutoka sare katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Mchezo huo uliwafanya Mzamiru Yassin nw Shiza Kichuya kucheza kwa mara ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mara ya kwanza tangu wasajliwe Simba msimu huu wa dirisha la usajili.
Ibrahim Mohamed ni mchezaji mwingine ambaye alisajiliwa Simba msimu huu akitokea Mtibwa lakini hakupata nafasi ya kucheza.
Dondoo kwa namba
30 Namba kubwa zaidi ya jezi ilivaliwa na golikipa wa Mtibwa Sugar.
10 Pointi ambazo Simba imefikisha baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa.
6 Pointi za Mtibwa baada ya kucheza mechi nne. Imeshinda mechi mbili na kupoteza michezo miwili.
Katika mechi saba zilizopita, Mtibwa haijapata ushindi ushindi dhidi ya Simba. Imetoka sare kwenye mechi mbili na kupoteza mechi tano.
Maoni
Chapisha Maoni