Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mwasiti kufungua NGO ya mambo ya elimu



Msanii mkongwe wa muziki Mwasiti Almas ameweka wazi mpango wake wa kufungua NGO ambayo itakuwa inasaidia vijana wa kike katika ya elimu.
Mwasiti
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Unaniangalia’ amesema baada ya kufanya kazi ‘Sister Tanzania’ ameona vijana wengi wanakosa elimu kutokana na changamoto mbalimbali.
“Ili kudhibitisha kwamba napenda kujitolea kwa jamii katika siku za hivi karibuni natarajia kufungua NGO ya mambo ya elimu na ninaamini nitaifikia namba kubwa ya vijana wa Tanzania,” Mwasiti aliliambia gazeti la Mtanzania. “Lengo langu ni kuwatoa vijana sehemu moja na kuwapeleka nyingine kupitia elimu itakayokuwa naitoa maana wapo watu wanatamani kufika mahali nilipo lakini hawajui namna ya kufika… hii haitakuwa mara yangu ya kwanza kwa sababu nimefanya kazi na Sister Tanzania na nimepata uzoefu wa kutosha. Mfano kuna mambo ambayo kama msanii nikimwambia mtoto inakuwa rahisi kutekeleza kuliko akiambiwa na wazazi wake.”
Muimbaji huyo alisema atadili na wanawake wenzake, kwasababu kwake inakuwa rahisi zaidi kutoa elimu.
Alisema alipenda iwe kwa wanaume pia lakini atashindwa kwa kuwa kuna mambo atashindwa kuyazungumza na watoto wa kiume kutokana na utofauti wa kijinsia.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO.

 Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na  Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.  Profesa Saber  M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo leo.   Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifan...

SOMA BIBLIA TAKATIFU HAPA

                                                        BONYEZA HAPA KUSOMA BIBLIA       

AZAM ACADEMY MABINGWA MICHUANO YA AFRIKA MASHARIKI

TIMU ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam FC Academy’, usiku wa leo imefanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki ‘Azam Youth Cup 2016’ baada ya kuichapa Ligi Ndogo Academy kutoka Kenya mabao 3-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex. Azam Academy inatwaa ubingwa huo ikiwa imefikisha jumla ya pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza nyingine zikiwa dhidi ya Future Stars Academy kutoka Arusha (4-1) na Football for Good Academy ya Uganda (5-1). Kikosi kizima cha Azam Academy na viongozi wao wakiwa na Kombe lao Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba (kulia) akimkabidhi tuzo mchezaji Shaaban Iddi baada ya kuibuka mfungaji bora Shujaa wa mabingwa hao kwenye mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wake hatari Shaaban Idd aliyepachika wavuni mabao mawili kwa ustadi mkubwa dakika ya 15 na jingine 90, alilolifunga kwa staili ya ‘tik-tak’ huku bao jingine likifungwa na mshambuliaji mwingine hodari w...