Panapo majaaliwa, Tanzania inaweza ikawa na mchezaji atakayepiga na klabu ya Chelsea ya Uingereza.
Abbas ‘Barthez’ Pira akiwa kwenye majaribio Stanford Bridge
Abbas ‘Barthez’ Pira amechukuliwa kufanyiwa majaribio na klabu ya Chelsea inayomilikiwa na bilionea wa Urusi, Roman Abramovich.
Barthez akisikiliza maelekezo ya kocha
Pira ni mlinda mlango aliyewahi kuichea Coastal Union ya Tanga.
Kutokana na uwezo wake katika kupangua mashuti anapokuwa golini, mchezaji huyo kijana aliitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kikijiandaa na kuchuana na Chad kwenye mchezo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) kabla ya Chad kujitoa.
Na mwezi huu, Septemba, Pira ameanza taratibu kuiishi ndoto yake ya muda mrefu – kuchezea Chelsea.
“Finally made it to Chelsea FC trialist. Proud to be a first Tanzanian to go on Trial at Chelsea FC,” ameandika kwenye Twitter.
Tazama picha zake zaidi.
Maoni
Chapisha Maoni