Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni ambazo zinazodai kuwa makamu huyo wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameomba kujiuzulu nafasi yake hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo, habari hizo zilizoenezwa mitandaoni ni za uzushi na uongo kwa kuwa zinalenga kuleta uchochezi na kuliweka taifa kwenye taharuki.
Taarifa ya ofisi hiyo imeendelea kwa kuwataka wananchi wote kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya viongozi hao wa serikali ya awamu ya tano.
Wakati huo huo ofisi hiyo imewataka watanzania wote kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.
Maoni
Chapisha Maoni