Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Wanafunzi 3918 wachaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa awamu ya pili


WANAFUNZI 3,918 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kujaza nafasi zilizokuwa wazi kutokana na ufinyu wa nafasi na baadhi ya wanafunzi kutoripoti kwa wakati.

Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe ilisema kati ya wanafunzi hao wasichana ni 2,413 na wavulana 1,505.

“Kuchaguliwa kwa wanafunzi hao kumefuatia kuwapo kwa nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni tangu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika awamu ya kwanza” alisema Mhandisi Iyombe.

Aidha Mhandisi Iyombe alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 1,864 sawa na asilimia 47.58 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo kati yao   wasichana 1,099 na wavulana 765.

Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa katika masomo ya Sanaa na Biashara wanafunzi takribani 2,054 (52.42%) wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo, ambapo kati yao wasichana ni 1,314 na wavulana 740.

“Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii” alisema Mhandisi Iyombe.
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO.

 Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na  Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.  Profesa Saber  M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo leo.   Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifan...

SOMA BIBLIA TAKATIFU HAPA

                                                        BONYEZA HAPA KUSOMA BIBLIA       

AZAM ACADEMY MABINGWA MICHUANO YA AFRIKA MASHARIKI

TIMU ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam FC Academy’, usiku wa leo imefanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki ‘Azam Youth Cup 2016’ baada ya kuichapa Ligi Ndogo Academy kutoka Kenya mabao 3-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex. Azam Academy inatwaa ubingwa huo ikiwa imefikisha jumla ya pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza nyingine zikiwa dhidi ya Future Stars Academy kutoka Arusha (4-1) na Football for Good Academy ya Uganda (5-1). Kikosi kizima cha Azam Academy na viongozi wao wakiwa na Kombe lao Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba (kulia) akimkabidhi tuzo mchezaji Shaaban Iddi baada ya kuibuka mfungaji bora Shujaa wa mabingwa hao kwenye mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wake hatari Shaaban Idd aliyepachika wavuni mabao mawili kwa ustadi mkubwa dakika ya 15 na jingine 90, alilolifunga kwa staili ya ‘tik-tak’ huku bao jingine likifungwa na mshambuliaji mwingine hodari w...