Taarifa ya Klabu hiyo imesema Jonathan Heimes enzi za uhai wake alichangisha maelfu ya Euro kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa Saratani ambapo shabiki huyo alikufa kwa ugonjwa wa saratani akiwa na umri wa miaka 26.
Uwanja huo ambayo unajulikana kwa jina la The Merck-Stadion am Boellenfalltor sasa utatambulika kwa jina la Jonathan-Heimes Stadion am Boellenfalltor kwa kipindi cha mwaka mmoja msimu wa 2016-17.
Nahodha wa klabu hiyo Aytac Sulu amekaririwa akisema kwamba "kila anayejitambulisha nasi anajitambulisha na Jonathan,".
Naye mzazi wa Heimes Martin amesema klabu hiyo na wadhamini wake wameonesha tendo kuu.
Maoni
Chapisha Maoni