Ronaldo alikunja sura kuonesha kuchukizwa na maamuzi ya Zidane kuhusu kumpumzisha.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ronaldo kupumzishwa kwa sababu za kiufundi wakati wa mchezo mgumu.
Wakati Ronaldo anapumzishwa dakika ya 72, Real Madrid ilikuwa inaongoza kwa 2-1 mbele ya Las Palmas. Zikiwa zimesalia dakika 5 mechi kumalizika, Las Palmas wakasawazisha kwa goli la Sergio Araujo.
Mwisho wa mchezo, Real Madrid ikapoteza pointi mbili wakati ilikuwa ikipambana kurejea kileleni mwa La Liga baada ya Barcelona kushinda 5-0 kwenye mechi yao ya mchana.
Maoni
Chapisha Maoni