Leicester City wanataka pauni milioni 45 kumuuza Riyad Mahrez, 25, lakini wana uhakika kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria atabakia King Power Stadium hasa baada ya kuondoka kwa N'Golo Kante kwenda Chelsea (Telegraph), Manchester United wamechelewesha kutangaza namba za jezi za wachezaji wake kwa msimu mpya mpaka watakapokamilisha usajili wa pauni milioni 105 wa kiungo wa Ufaransa na Juventus, Paul Pogba, 23 (Sun), mwenyekiti wa West Ham, David Sullivan, amesema mshambuliaji Diafra Sakho, 26, haondoki labda timu hiyo ipate mchezaji atakayeweza kuziba pengo lake (Mirror), Arsenal wanapanga kusajili wachezaji wawili kwenye safu ya ulinzi, wakimtaka Jason Denayer, 21 kutoka Manchester City na Matthias Ginter, 22 kutoka Borussia Dortmund (Sun), Bayern Munich na Real Madrid bado wanamfuatilia winga anayesakwa na Manchester City, Leroy Sane, 20, kwa mujibu wa baba wa mchezaji huyo kutoka Ujerumani (Manchester Evening News), dau la Arsenal la pauni milioni 2 limek