MSHAMBULIAJI WA ZAMAN WA CHELESEA YA UINGEREZA KATIKA LIG KUU YA UINGEREZA
Demba Ba avunjika mguu uwanjani !
Mshambulizi wa
zamani wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Demba Ba amevunjika mguu akiwa
uwanjani katika mechi ya ligi kuu ya Uchina.
Raia huyo wa Senegal
mwenye umri wa miaka 31 alikabiliwa na mlinzi wa timu hasimu katika ligi
kuu ya Uchina hapo jana Jumapili tarehe 17 Julai.Ba ambaye anaichezea Shanghai Shenhua aligongwa na mchezaji wa timu hasimu ya Shanghai SIPG mita chache tu kabla ya kisanduku cha hatua 18, Alipoanguka mguu wake ulipinduka kwa hali isiyo ya kawaida na kuvunjika papo hapo.
Video ya mechi hiyo inaogofya haswa inavyoonesha wazi wazi mguu wake umevunjika kati ya goti na kisigono.
Kocha wa klabu yake Gregorio Manzano ameonya kuwa tukio hilo linaweza kumlazimisha nyota huyo kustaafu kucheza soka .
Maoni
Chapisha Maoni