Morroco imetoa tamko la nia yake ya
kutaka kujiunga tena katika umoja wa Afrika.katika ujumbe ulitumwa
kutoka kwenye mkutano wa Umoja wa Matataifa nchini Rwanda,mjini
Kigali,Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita amesema sasa ni wakati muafaka
kwa taifa lake kurejea na kuchukua nafasi yake katika jumuiya hiyo ya
umoja wa Afrika.
Morocco ilijitoa katika umoja huo
mwaka 1984 wakati umoja huo ulipotambua uhuru wa eneo la magharibi mwa
sahara.Ambapo Morocco ilidai kuwa eneo la magharibi mwa sahara lilikuwa
ndani ya mipaka yake.
Hata hivyo Umoja wa Afrika umesema
utaendelea kusukuma upatikanaji wa haki ya watu wa eneo la Magharibi mwa
Sahara ili kuwa na uhuru kamili bila kuingiliwa.BBC
Maoni
Chapisha Maoni