Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2016

COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili  katika Klabu ya Coastal Union,Hemed Aurora akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketijuzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo,kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo,Abdallah Zuberi,kulia ni Hussein Chuse na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri,   Mjumbe wa Kamati ya Mashindano namUsajili ya Klabu ya Coastal Union,Steven Mguto akiuliza swali wakati wa kikao cha kamatihiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketi juzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union,Salim Bawaziri akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao hicho  Kamati hiyo inaundwa na wajumbe  wengine ambao ni Abdi Masamaki,Salim Bawaziri,Hemed Mbaruku,Hussein  Chuse,Abdallah Zuberi “Unenge” na Juma Mgunda ambayo itakuwa na jukumu  la kusimamia mashindano na usajili. Picha kwa hisani ya kitengo

ASKARI AKUTWA NA KESI YAKUJIBU MAUWAJI YA MWANGOSI

 Daud Mwangosi enzi za uhai wake. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mjini Iringa, Pasificus Cleophace Simon katika kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha Channel Ten, Daud Mwangosi. Daud Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Mwangosi kabla ya kuuawa.

MESS AWEKA REKODI MPYA YA UFUNGAJI

Lionel Mesi  sasa anaongoza orodha ya wafungaji katia taifa la Argentina baada ya kuopiga mkwaju wa free-kick uliozama moja kwa moja kambani wakati Argentina ikiiangamiza USA kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa nusu fainali kisha kufuzu fainali ya Copa America kwa mara ya pili mfululizo. Star huyo wa Barcelona ameivunja rekodi ya Gabriel Batistuta ya magoli 54 baada ya kufunga bao lake la 55 kwa mkwaju wa adhabu ndongo umbali wa mita 25 kwenye ushindi wa Argentina wa magoli 4-0 dhidi ya United States. Messi alisaidia kupatikana kwa bao la kwanza lililofungwa na Ezequiel Lavezzi, kisha akafunga bao la pili kabla ya striker wa Napoli Gonzalo Higuain kupachika bao jingine ma kuiweka mbele Argentika kwa bao 3-0. Higuain alifunga bao jingine dakika ya 85 kumaliza mchezo huo uliowapeleka hatua ya fainali. “Nimefurahi kuivunja rekodi ya Batistuta  na nawashukuru wachezaji wenzangu ni rekodi yao pia,” amesema Messi ambaye Ijumaa atafikisha miaka 29. Argentina itacheza fainali dhidi ya Colombia au

TFDA YAKAMATA ZAIDI YA TANI SITA ZA TENDE ZILIZO HIFADHIWA KWENYE MADEBE

Mamlaka ya chakula na dawa nchini tawi la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania imekamata shehena ya bidhaa aina ya tende zaidi ya tani sita zilizokuwa zikitokea uarabuni kupitia nchi jirani ya Kenya kufuatia bidhaa hizo zilizokuwa zikiletwa nchini kwa ajili ya matumizi ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuhifadhiwa katika madebe yanayodaiwa kuwa yanaweza kuleta madhara kwa mtumiaji. Akizungumza na ITV katika eneo la Horohoro mpakani mwa  Kenya na Tanzania mkaguzi wa mamlaka hiyo katika mpaka huo Thomas Nkondola amesema zipo baadhi ya tende ambazo zinaingizwa kutoka uarabuni kupitia nchi jirani ya Kenya zinakuwa na nembo ya ubora na kufungashwa katika vifungashio ambavyo havina madhara na wanaziruhusu tofauti na hizo zilizokamatwa. Baadhi ya watumiaji wa bidhaa hiyo ya tende waliokutwa katika mpaka huo wamesema baadhi yao walitumia tende zilizofungashwa katika madebe waliathirika afya zao kwa kushikwa na homa za matumbo hatua ambayo wameshauriwa na daktari kuwa bidhaa hiyo isitumike kw

WAGONJWA WA LALAMIKIA UKOSEFU WA LIFT KWENYE HOSPITALI YA (MOI)

Ukosefu wa Lift katika jengo la wagonjwa la taasisi ya mifupa ya MOI katika Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam umeelezwa kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili wagonjwa wanaofika katika kitengo hicho kwa ajili ya kupata matibabu. Muonekano wa jengo bora na imara la kitengo cha mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, ambalo ukosefu wa lift licha ya kuwa mwiba kwa wagonjwa. Ambapo  mmoja wa wauguzi wa jengo hilo ambaye tunahifadhi jina lake ameieleza ITV madhira wanayoyapata kuwapandisha wagonjwa kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya tano kwa kutumia ngazi. Huku tukipiga picha kwa usiri, tulizungumza na mmoja wa mafundi wa kampuni ya Premider Elevetor ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake ambapo amesema wameamua kusitisha utoaji huduma wa Lift kutokana deni kubwa wanaloidai taasisi hiyo, na kwamba watafanya hivyo mpaka pale deni lao litakapolipwa. Lakini uongozi wa taasisi hiyo ya mifupa ya MOI umesisitiza hakuna tatizo la Lift katika jengo hilo,huku wag

SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MNASA MWENGINE ALIYE MTUKANA RAIS MAGUFUL KWENYE WHATSAPP

Sheria ya makosa ya mtandao imemng’ata mtu mwingine. Leonard Mulokozi Kyaruzi anakabiliwa na kesi baada ya kuandika maneno ya kumtukana Rais John Pombe Magufuli si kwenye Facebook kama Isaac Abubakar wa Arusha, bali ni kwenye WhatsApp – Yes ulidhani kwenye magroup unaweza kutukana unavyotaka? Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyotolewa Jumanne hii, Kyaruzi anadaiwa kutoa kauli hiyo ya kejeli kwenye WhatsApp June 2. Aliandika: Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu? Bwege sana huyu jamaa, he doesn’t consider the law in place before opening his mouth!. Au na yeye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?” Kyaruzi anakabiliwa na kosa lile lile aliloshtakiwa Isaac miezi kadhaa iliyopita, Hata hivyo yeye alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni 7. Alichangiwa kiasi hicho cha fedha na kukilipa na sasa ni mtu huru.

WAZIRI MWAKIEMBE KULISHITAKI GAZETI LA DIRA LILILOSEMA AMETAPELI BILION 2

Waziri Mwakyembe kulishitaki gazeti la Dira lililosema ametapeli bilioni 2 June 21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi. "Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu " Amesem a waziri Mwakyembe na kuongeza "Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji "Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema ki

POLIS WAKAMATA RISAS 853 ZILIZOFICHWA KWENYE DUMU

JESHI la Polisi mkoani Morogoro, limekamata risasi 853 zinazotumika kwenye silaha aina ya G3 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye dumu la lita 20 pembeni mwa mto Ngerengere eneo la Kihonda. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira ametoa taarifa kwa waandishi wa habari  akisema risasi hizo zilikamatwa jana jioni eneo la Kihonda Kilimahewa. Rwegasira amesema polisi wakiwa katika utekelezaji wa mapambano dhidi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kwa kufanya msako maeneo mbalimbali ndipo walipopata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna risasi zimehifadhiwa na watu wasiojulikana pembezoni mwa mto huo.
MACHINGA JIJINI MWANZA WAKUTANA KUAMUA HATIMA YAO Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo. Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Machinga Mkoa wa Mwanza SHIUMA, ulilenga kujadiliana na wadau wengine wa Uwekezaji ikiwemo taasisi za kifedha, juu ya Kurasimisha biashara zao na kuwekwa kwenye mifumo rasmi ya Kibiashara na Kijamii. Machinga wamesema changamoto kubwa zinazowakabiri ni Ukosefu wa Mitaji ya Biashara, Maeneo ya Kufanyia Biashara pamoja na Ukosefu wa Elimu Biashara. Wamesema wanataka nao watambulike na taasisi za kifedha ili wapate fursa ya kukopesheka ili kukuza mitaji yao.

SERIKALI YA FUTA UTARATIBU ILIOUPENDEKEZA KWA TAASISI ZA DINI KULIPA KODI KABLA KWA BIDHAA WATAKAZO NUNUA

Serikali Yafuta Utaratibu Ilioupendekeza Kwa Taasisi Za Dini Kulipa Kodi Kwanza Kwa Bidhaa Watakazonunua Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip mpango amesema amefuta utaratibu alioupendekeza bungeni wa taasisi za dini kulazimika kulipa kodi kwanza kwa bidhaa watakazonunua au kuagiza nje na kodi hiyo kurejeshwa baada ya ukaguzi kufanyika. Waziri Mpango ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wabunge kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Amesema kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji huduma za elimu na afya anapendekeza kufuta utaratibu huo na badala yake Serikali itaimarisha zaidi hatua mbalimbali za udhibiti wa msamaha ya kodi.

HABARI ZA USAJILI ULAYA

HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 19,2016. Daley Blind Blind:Arsenal imepania kufanya makubwa msimu ujao na katika kuona hilo linafanikiwa imeanza jitihada za kutaka kumsajili staa wa Manchester United mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani,Mholanzi Daley Blind. Arsenal imeamua kumgeukia Blind,26, baada ya kuona kuwa staa huyo wa zamani wa Ajax atakuwa na wakati mgumu wa kupata namba Old Trafford hasa baada ya ujio wa mlinzi Eric Bailly kutoka Villarreal.  (Mirror) Mane:Southampton haitaki kuona winga wake mahiri Msenegal Sadio Mane,23, anaondoka klabuni hapo na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa imepandisha bei yake mpaka kufikia £40m kama mbinu ya kuvivunja nguvu vilabu vyote vinavyomtaka staa huyo wa zamani wa Redbull Salzburg.  (The Sun) Bonucci:Meneja wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho ameonyesha kuvutiwa na mlinzi wa Juventus, Leonardo Bonucci,29, na ameripotiwa kutaka kumsajili kwa dau la £

WAZIRI WA MICHEZO NAPE NNAUYE ASHIRIKI SIKU YA KIMATAIFA YA YOGA

WAZIRI WA MICHEZO NAPE NNAUYE ASHIRIKI SIKU YA KIMATAIFA YA YOGA.   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimia na Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Coco kushiriki Siku ya kimataifa ya Yoga leo June 19, 2016.   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi Peter Kallaghe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika viwanja vya Coco kwenye hafla ya    kuadhimisha   Siku ya kimataifa ya    Yoga leo June 19, 2016.   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco leo June 19, 2016 kushoto ni Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya .   Balozi wa India nchini Mhe. Sandip Arya akizungumza katika Siku ya Kimataifa ya Yoga iliyofanyika katika viwanja vya Coco leo June 19, 2016 kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mich

WAPEWA WIKI MBILI KUPELEKA WATOTO SHULE

chunya; uongozi wa serikali katka wilaya ya  chunya mkoani mbeya ume wataka wazazi kuhakikisha wanarudisha wanafunzi wote walio kimbia masomo kuanzia sasa had julai 1 mwaka huu.                                          uongozi huo umesems baada ya  hapo utafanyika  msako wakubaini ambao hawakutekeleza agizo hilo nakufishwa kwenye vyombo vya dola                                                      OFISA tawala wa wilaya hiyo SOstenes mayoka ametoa kauli hiyo kikao cha wazazi cha kupanga mikakati  ya kuinua kiwango cha elimu wilayani hapa katka kijiji cha itumbikata ya matumbas             ''hatutakikuendelea kushuhudia lundo la vijana wasio kuwa na elimu wako mitaan na ninyi wazazi mnao ruhusu watoto wenu kwenda kwenye machimbo badala ya kuwatengenezea mazingira bora ya kwenda shule kiama chenu kina sogea ''amesema mayoka.