Akizungumza na ITV katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania mkaguzi wa mamlaka hiyo katika mpaka huo Thomas Nkondola amesema zipo baadhi ya tende ambazo zinaingizwa kutoka uarabuni kupitia nchi jirani ya Kenya zinakuwa na nembo ya ubora na kufungashwa katika vifungashio ambavyo havina madhara na wanaziruhusu tofauti na hizo zilizokamatwa.
Baadhi ya watumiaji wa bidhaa hiyo ya tende waliokutwa katika mpaka huo wamesema baadhi yao walitumia tende zilizofungashwa katika madebe waliathirika afya zao kwa kushikwa na homa za matumbo hatua ambayo wameshauriwa na daktari kuwa bidhaa hiyo isitumike kwa matumizi ya binadamu.
Kufuatia hatua hiyo mkaguzi mkuu wa (TFDA) tawi la Horohoro Bwana Nkondola amewashauri watumiaji kuwa makini na bidhaa aina ya tende ambazo zimeingizwa katika njia zisizo rasmi huku mamlaka hiyo ikiendelea kuzuia zile ambazo zimehifadhiwa katika madebe ambayo yanahifadhi kutu ambayo ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
Maoni
Chapisha Maoni