Leonard Mulokozi Kyaruzi anakabiliwa na kesi baada ya kuandika maneno ya kumtukana Rais John Pombe Magufuli si kwenye Facebook kama Isaac Abubakar wa Arusha, bali ni kwenye WhatsApp – Yes ulidhani kwenye magroup unaweza kutukana unavyotaka?
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyotolewa Jumanne hii, Kyaruzi anadaiwa kutoa kauli hiyo ya kejeli kwenye WhatsApp June 2. Aliandika: Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu? Bwege sana huyu jamaa, he doesn’t consider the law in place before opening his mouth!. Au na yeye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?”
Kyaruzi anakabiliwa na kosa lile lile aliloshtakiwa Isaac miezi kadhaa iliyopita, Hata hivyo yeye alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi milioni 7. Alichangiwa kiasi hicho cha fedha na kukilipa na sasa ni mtu huru.
Maoni
Chapisha Maoni