Ruka hadi kwenye maudhui makuu

WAGONJWA WA LALAMIKIA UKOSEFU WA LIFT KWENYE HOSPITALI YA (MOI)


Ukosefu wa Lift katika jengo la wagonjwa la taasisi ya mifupa ya MOI katika Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam umeelezwa kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili wagonjwa wanaofika katika kitengo hicho kwa ajili ya kupata matibabu.

Muonekano wa jengo bora na imara la kitengo cha mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam, ambalo ukosefu wa lift licha ya kuwa mwiba kwa wagonjwa.

Ambapo  mmoja wa wauguzi wa jengo hilo ambaye tunahifadhi jina lake ameieleza ITV madhira wanayoyapata kuwapandisha wagonjwa kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya tano kwa kutumia ngazi.

Huku tukipiga picha kwa usiri, tulizungumza na mmoja wa mafundi wa kampuni ya Premider Elevetor ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake ambapo amesema wameamua kusitisha utoaji huduma wa Lift kutokana deni kubwa wanaloidai taasisi hiyo, na kwamba watafanya hivyo mpaka pale deni lao litakapolipwa.

Lakini uongozi wa taasisi hiyo ya mifupa ya MOI umesisitiza hakuna tatizo la Lift katika jengo hilo,huku wagonjwa wakisema Lift ni changamoto kuu kwa wiki sita sasa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMA BIBLIA TAKATIFU HAPA

                                                        BONYEZA HAPA KUSOMA BIBLIA       

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO.

 Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na  Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.  Profesa Saber  M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo leo.   Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa.  Kutoka kushoto ni

UNGANA NA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE KATIKA KUABUDU.UNGANA NAE UBARIKIWE.