HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA ULAYA JUMAPILI YA LEO JUNI 19,2016.
Daley
Blind Blind:Arsenal imepania kufanya makubwa msimu ujao na katika kuona
hilo linafanikiwa imeanza jitihada za kutaka kumsajili staa wa
Manchester United mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi
uwanjani,Mholanzi Daley Blind.
Arsenal
imeamua kumgeukia Blind,26, baada ya kuona kuwa staa huyo wa zamani wa
Ajax atakuwa na wakati mgumu wa kupata namba Old Trafford hasa baada ya
ujio wa mlinzi Eric Bailly kutoka Villarreal. (Mirror)
Mane:Southampton haitaki kuona winga wake mahiri Msenegal Sadio
Mane,23, anaondoka klabuni hapo na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa
imepandisha bei yake mpaka kufikia £40m kama mbinu ya kuvivunja nguvu
vilabu vyote vinavyomtaka staa huyo wa zamani wa Redbull Salzburg. (The
Sun) Bonucci:Meneja wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho ameonyesha
kuvutiwa na mlinzi wa Juventus, Leonardo Bonucci,29, na ameripotiwa
kutaka kumsajili kwa dau la £25m. (Daily Star) Wenger:Arsenal iko tayari kumpa mkataba mpya wa miaka miwili meneja wake Mfaransa Arsene Wenger,66. (Mirror)
Dzeko:Sunderland imechoka kuwa timu ya kukoswa koswa kushuka daraja
karibu kila msimu na tayari imetuma ofa ya €11m kwenda AS Roma kwa ajili
ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester City,Mbosnia
Edin Dzeko lakini italazimika kutoa kitita cha €15m ili kuishawishi
miamba hiyo ya Estadio Olympic.(gianlucadimarzio.com) Kovacic:Liverpool
imeungana na vilabu vya Juventus, Roma na AC Milan kuwania kumsajili kwa
mkopo kiungo wa Real Madrid,Mcroatia Mateo Kovacic,22.(Sky Sport
Italia) Nolito:Mwenyekiti wa Celta Vigo, Carlos Mourino amesema staa wa
klabu hiyo Muhispania Manuel Arago maarufu kama Nilito,29, anaweza
kuihama klabu hiyo katika kipindi hiki cha usajili kwa ada ya €18m
(£13.8m).
Maoni
Chapisha Maoni