Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2016

Kijana aliye na jinsia mbili aliyesoma katika shule ya wasichana

-Kijana mmoja amekuwa akiishi kama ‘mwanamke’ kwa miaka. -Kijana huyo alisoma katika shule za wasichana na hata kupewa jina la kike. Mvulana mmoja kutoka Naivasha anayejulikana kama Mary Waithera, na ambaye amekua akiishi kama msichana sasa anataka kubalisha majina yake na kujiita James Karanja. Kijana aliye na jinsia mbili aliyesoma katika shule ya wasichana Waithera alizaliwa na jinsia mbili miaka ishirini iliyopita na sasa amekugundua kwamba ana wingi wa jinsia za kiume kuliko  za kike. Cira,kama vile anavyoitwa na wenzake aliishi na nyanyake tangu utotoni  na anasema kwamba nyanya ndiye alimzoesha kwa kumvalisha mavazi ya wasichana. Baada ya kufanya mtihani wake wa darasa la nane, Waithera alijiunga na shule ya upili ya wasichana ya Kambala katika eneo la Molo, nakueleza kuwa wanafunzi wenzake walimkejeli kwa kumpa jina la utani la ‘Mary boy.’ Wakiongea kwenye Runinga ya Inooro ,waalimu wake walisema hawakujua chochote cha ajabu kwa waithera isipo

Kocha wa Al Ahly ajiuzulu akihofia usalama

  Mholanzi Martin Jol Mkufunzi mkuu wa klabu ya Al Ahly ya Misri amejiuzulu chini ya mwaka mmoja baada ya kuteuliwa kuongoza klabu hiyo. Mholanzi Martin Jol amejizulu baada ya kuhudumu kwa miezi sita pekee akisema anahofia usalama wake. Mashabiki wa klabu hiyo walionekana kukerwa sana na kushindwa kwa timu hiyo kufika hatua ya nusufainali Ligi ya Mabingwa Afrika. Jol alijibizana na mashabiki Ijumaa iliyopita baada ya timu yake kutoka sare 2-2 na klabu ya Zesco United na kuzima matumaini yao ya kusonga mbele. Tangu wakati huo amepokea vitisho pia kupitia mitandao ya kijamii jambo ambalo anasema limechangia uamuzi wake wa kuondoka.

Olimpiki Rio 2016: Matukio yaliyosisimua zaidi

Mshirikishe mwenzako Michezo ya Olimpiki Rio 2016 ilishuhudia matukio mengi ya kukumbukwa, baadhi mazuri na mengine mabaya. Haya hapa ni baadhi ya mambo yatakayokumbukwa sana. Mbeba bendera wa Tonga Pita Taufatofua alivutia wengi kwa mtindo wake wa mavazi sherehe ya ufunguzi. Taufatofua, mchezaji aliyesisimua kwa mavazi Rio Picha moja iliyodhirisha tofauti katika kimo na unene ilikuwa hii ya mwanamichezo ya mazoezi ya viungo kutoka Marekani Ragan Smith na mchezaji mpira wa kikapu DeAndre Jordan. Mwanaolimpiki anayefanana nawe Rio Kulikuwa pia na kisa cha urafiki licha ya uadui wa mataifa. Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Korea Kaskazini, wachezaji wawili wa mazoezi ya viungo ambao nchi zao ni mahasimu wakuu, walipiga picha pamoja. Wachezaji wa Korea

Mpiganaji wa Kiislamu Mali akiri makosa ICC

, 40, ni mshukiwa wa kwanza kukiri makosa ICC Mpiganaji wa Kiislamu amekiri makosa ya kuharibu maeneo yenye umuhimu mkubwa kitamaduni katika mji wa Timbuktu, Mali baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Ahmad al-Faqi al-Mahdi amesema anajutia vitendo vyake. Ameshtakiwa kuongoza waasi ambao waliharibu turathi muhimu kihistoria mwaka 2012. Hii ni mara ya kwanza kwa mpiganaji wa Kiislamu kufikishwa kortini katika ICC na pia mara ya kwanza kwa mshukiwa kukiri mashtaka. Viongozi wa amshtaka wamesema Mahdi alikuwa mwanachama wa kundi la Kiislamu la Ansar Dine ambalo liliteka na kudhibiti mji wa Timbuktu kwa miezi kadha. Waislamu huamini madhabahu pamoja na miswada ya kale ya mji huo ambayo huangazia mambo mengi yakiwemo historia na utaalamu wa nyota na sayari kuwa uabudu sanamu. Nyaraka za mahakama zinamueleza Mahdi, 40, kama msomi wa kidini aliyewaongoza

MREMBO AGNES MASOGANGE AZIDI KUZIHILISHA UZURI WAKE(+PICHAZ)

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO.

 Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na  Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.  Profesa Saber  M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo leo.   Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa.  Kutoka kushoto ni

TANGA YAANZA MAANDALIZI MRADI WA BOMBA LA MAFUTA.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, akiongea jambo mara baada ya kutembelea eneo la Chongoleani Mkoani Tanga, itakapojengwa Gati itakayotumika kupakua mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda.  Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Martine Shigella ( Wa tano kutoka kulia), katika picha ya pamoja  na  Wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Bandari Tanga . Pia yupo Meya wa Jiji la Tanga na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.  Mkurugenzi wa Sheria, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ibrahim Ngabo, akizungumza na waandishi wa Habari wakati Mkuu wa Mkoa wa Tanga alipotembelea eneo la Chongoleani itakapojengwa gati itakayotumika kupakua mafuta ghafi. Maandalizi ya awali ya kuandaa eneo itakapojengwa Gati itakayotumika kupakua mafuta ghafi ya kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga yakiendelea. Picha kwa Hisani ya www.tangaraha.tz.blogspot.com Na Asteria Muhozya, Tanga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigell

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU JIJINI DAR KUWAANDAA KUHAMIA DODOMA

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi yake kuhusu utaratibu wa kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016.  Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kuhusu utaratibu wa kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2016  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akizungumza katika Mkutano wa  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu  Agosti 17, 2016  kuhusu Utaratibu wa kuhamia Dodoma.    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi  zilizoko chini ya Ofisi yake baada ya kuzungumza na watumishi wa Ofisi yake kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana  Ajira na Walemavu, Jenista  Mhagama , Wapili kulia kwake ni