Mkufunzi mkuu wa klabu ya Al Ahly ya Misri amejiuzulu chini ya mwaka mmoja baada ya kuteuliwa kuongoza klabu hiyo.
Mholanzi Martin Jol amejizulu baada ya kuhudumu kwa miezi sita pekee akisema anahofia usalama wake.Mashabiki wa klabu hiyo walionekana kukerwa sana na kushindwa kwa timu hiyo kufika hatua ya nusufainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Jol alijibizana na mashabiki Ijumaa iliyopita baada ya timu yake kutoka sare 2-2 na klabu ya Zesco United na kuzima matumaini yao ya kusonga mbele.
Tangu wakati huo amepokea vitisho pia kupitia mitandao ya kijamii jambo ambalo anasema limechangia uamuzi wake wa kuondoka.
Maoni
Chapisha Maoni