Mpiganaji wa
Kiislamu amekiri makosa ya kuharibu maeneo yenye umuhimu mkubwa
kitamaduni katika mji wa Timbuktu, Mali baada ya kufikishwa katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Ahmad al-Faqi al-Mahdi amesema anajutia vitendo vyake.Ameshtakiwa kuongoza waasi ambao waliharibu turathi muhimu kihistoria mwaka 2012.
Hii ni mara ya kwanza kwa mpiganaji wa Kiislamu kufikishwa kortini katika ICC na pia mara ya kwanza kwa mshukiwa kukiri mashtaka.
Viongozi wa amshtaka wamesema Mahdi alikuwa mwanachama wa kundi la Kiislamu la Ansar Dine ambalo liliteka na kudhibiti mji wa Timbuktu kwa miezi kadha.
Waislamu huamini madhabahu pamoja na miswada ya kale ya mji huo ambayo huangazia mambo mengi yakiwemo historia na utaalamu wa nyota na sayari kuwa uabudu sanamu.
Nyaraka za mahakama zinamueleza Mahdi, 40, kama msomi wa kidini aliyewaongoza wapiganaji kutumia shoka na patasi kuharibu madhabahu hayo baada ya kushindwa kuwashawishi wakazi kuacha kuyatumia kama eneo la ibada.
Ameshtakiwa makosa ya uhalifu wa kivita kuhusiana na uharibifu uliotokea katika makarubi tisa na msikiti.
Mahdi ameambia ICC: "Ningependa kutoa ushauri wa Waislamu wote duniani, wasijihusishe na vitendo sawa na nilivyovifanya, kwa sababu havitakuwa na faida zozote kwa binadamu."
Baada yake kukiri makosa, huenda kesi yake ikamaliza kusikizwa kufikia mwisho wa wiki hii.
Anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha hadi miaka 30 jela.

Maoni
Chapisha Maoni