Michezo ya Olimpiki Rio 2016
ilishuhudia matukio mengi ya kukumbukwa, baadhi mazuri na mengine
mabaya. Haya hapa ni baadhi ya mambo yatakayokumbukwa sana.
Mbeba bendera wa Tonga Pita Taufatofua alivutia wengi kwa mtindo wake wa mavazi sherehe ya ufunguzi.
Picha moja iliyodhirisha tofauti katika kimo na unene ilikuwa hii ya mwanamichezo ya mazoezi ya viungo kutoka Marekani Ragan Smith na mchezaji mpira wa kikapu DeAndre Jordan.
Kulikuwa pia na kisa cha urafiki licha ya uadui wa mataifa. Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Korea Kaskazini, wachezaji wawili wa mazoezi ya viungo ambao nchi zao ni mahasimu wakuu, walipiga picha pamoja.
Lakini hakukuwa na urafiki wakati wowote. Twitter 'iliwaka moto' baada ya bingwa wa uoegeleaji Michael Phelps kuonekana akimwangalia vibaya mpinzani wake Chad le Clos.
Medali ya kwanza ya dhahau kwa wenyeji, iliyomwendea bingwa wa judo wa uzani wa kilo 57 Rafaela Silva, iliwapa kitulizo wakazi wa maeneo maskini Rio. Silva alizaliwa eneo maskini Rio na mwaka 2012 akatimuliwa mashindano London na kuelezwa kama "aibu kuu". Lakini mwaka huu ulikuwa wa fahari kwake.
helps, mwogeleaji aliyeshinda medali nyingi, hatimaye alitabasamu baada ya kumshinda Clos wa Afrika Kusini fainali za 200m butterfly wanaume. Baadhi walipendekeza Clos alifaa kuangazia kuogelea badala ya kumwangalia mpinzani wake.
Kulikuwa na mengine mazuri kando na ushindi. Rami Anis, mwogeleaji wa timu ya wakimbizi aliyetoroka Syria 2015 kwa boti na kupitia bahari ya Mediterranean hadi Uturuki alisifiwa sana baada ya kuandikisha muda wake bora zaidi 100m freestyle upande wa wanaume. picha zote kwa hisani ya bbc fwatialia zaidi kwenye bolg yako ya kijanja kwa taarifa mbalimbal yoas.tz
Maoni
Chapisha Maoni