-Kijana mmoja amekuwa akiishi kama ‘mwanamke’ kwa miaka.
-Kijana huyo alisoma katika shule za wasichana na hata kupewa jina la kike.
Mvulana mmoja kutoka Naivasha anayejulikana kama Mary Waithera, na ambaye amekua akiishi kama msichana sasa anataka kubalisha majina yake na kujiita James Karanja.
Kijana aliye na jinsia mbili aliyesoma katika shule ya wasichana
Waithera alizaliwa na jinsia mbili miaka ishirini iliyopita na sasa amekugundua kwamba ana wingi wa jinsia za kiume kuliko za kike.
Cira,kama vile anavyoitwa na wenzake aliishi na nyanyake tangu utotoni na anasema kwamba nyanya ndiye alimzoesha kwa kumvalisha mavazi ya wasichana.
Baada ya kufanya mtihani wake wa darasa la nane, Waithera alijiunga na shule ya upili ya wasichana ya Kambala katika eneo la Molo, nakueleza kuwa wanafunzi wenzake walimkejeli kwa kumpa jina la utani la ‘Mary boy.’
Wakiongea kwenye Runinga ya Inooro ,waalimu wake walisema hawakujua chochote cha ajabu kwa waithera isipokuwa maumbile yake.
Tayari kimekuwa kibarua kigumu kwake kupata kitambulisho kilicho na majina anayoyataka.
Maoni
Chapisha Maoni