Rashford amefichua beki anayemuogopa zaidi EPL 1 1 Marcus Rashford amemtaja Laurent Koscielny kama beki mgumu kabisa kuwahi kukutana naye mpaka sasa kwenye maisha yake ya soka. Rashford amekuwa kwenye kiwango bora tangu apate nafasi kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United msimu uliopita, akifunga mabao 12 kwenye michuano yote. Straika huyo amekuwa na tabia ya kufunga kila mechi katika michuano anayocheza kwa mara ya kwanza akiwa United na timu ya England. Ikumbukwe Rashford alifunga mabao mawili kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi ya England dhidi ya Arsenal ambapo United walishinda mabao 3-2 Old Trafford. Lakini Rashford (18), bado anaamini kwamba beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa ndiyo beki mgumu zaidi kuwahi kukutana naye. “Nadhani kwangu binafsi, Laurent Koscienly wa Arsenal,” Rashfod aliiambia tovuti rasmi ya United. “Ni beki mgumu zaidi kucheza naye.”
Marcus Rashford amemtaja Laurent Koscielny kama beki mgumu kabisa kuwahi kukutana naye mpaka sasa kwenye maisha yake ya soka.
Rashford amekuwa kwenye kiwango bora tangu apate nafasi kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United msimu uliopita, akifunga mabao 12 kwenye michuano yote.
Straika huyo amekuwa na tabia ya kufunga kila mechi katika michuano anayocheza kwa mara ya kwanza akiwa United na timu ya England.
Ikumbukwe Rashford alifunga mabao mawili kwenye mchezo wake wa kwanza kwenye Ligi ya England dhidi ya Arsenal ambapo United walishinda mabao 3-2 Old Trafford.
Lakini Rashford (18), bado anaamini kwamba beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa ndiyo beki mgumu zaidi kuwahi kukutana naye.
“Nadhani kwangu binafsi, Laurent Koscienly wa Arsenal,” Rashfod aliiambia tovuti rasmi ya United.
“Ni beki mgumu zaidi kucheza naye.”
Maoni
Chapisha Maoni