Vikosi vya usalama
nchini Uturuki vinasema kuwa zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi
wamefutwa kazi, kufuatia jaribio la mapinduzi lililozimwa wiki
iliyopita.Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa.
Fethullah Gulen amekanusha madai ya kuchochea mapinduzi
Msako dhidi ya maafisa wa usalama waliohusika na mipango ya kuipindua serikali juma lililopita nchini Uturuki, unaendelea.
Kituo cha mafunzo ya wanajeshi wa angani mjini cha Istanbul, kilivamiwa na maafisa hao kukamatwa.
Waendesha mashtaka wameanza kuwahoji kinara mkuu wa jaribio hilo la mapinduzi ambaye alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la angani Akin Ozturk, ambaye ni miongoni mwa makamanda wakuu 100 waliokamatwa.
Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao pia wamekamatwa.
Uturuki imeomba Ugiriki kuwarejesha nyumbani ili kushtakiwa, lakini mawakili wao wameomba idhini ya uhamiaji.
Maoni
Chapisha Maoni