Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AFCON 2017: TANZANIA BAIBAI AFRIKA, MISRI YATINGA FAINALI

TANZANIA  imetupwa rasmi ya nje ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2017 baada ya kuchapwa 2-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwenye Mechi ya Kundi G ambayo imeihakikishia Egypt kutinga Fainali huko Gabon Mwakani.
Kundi G limebakiwa na Timu 3 tu baada ya Chad kujitoa kutokana na ukata na sasa, baada ya kumaliza Mechi zao 4, Egypt wametwaa ushindi wa Kundi wakiwa na Pointi 10 wakifuatiwa na Nigeria wenye Pointi 2 baada ya Mechi 3 na Tanzania, waliocheza Mechi 3 pia, kuwa na Pointi 1.


Katika Mechi ya Leo Bao za Egypt zilifungwa na Profeshenali wao wa AS Roma Mohamed Salah Dakika za 44 na 59 huku Kepteni wa Taifa Stars Mbwana Samatta alikosa Penati Dakika ya 53.
KUNDI G - Msimamo:
AFCON2017-KUNDIG-MECHI4
++++++++++++++++++++++
AFCON 2017
**Timu zilizofuzu Fainali hadi sasa:
-Wenyeji Gabon
-Kundi C: Mali
-Kundi F: Morocco
-Kundi G: Egypt
-Kundi J: Algeria
-Kundi K: Senegal
-Kundi M: Cameroun
++++++++++++++++++++++
AFCON 2017
Ratiba/Matokeo:
Alhamisi Juni 2
Seychelles 0 Algeria 2
Ijumaa Juni 3
Djibouti 0 Tunisia 3
Mauritania 0 Cameroon 1
Libya 1 Morocco 1
Jumamosi Juni 4
Burundi 0 Senegal 2
Rwanda 2 Mozambique 3  
Botswana 1 Uganda 2
South Sudan 0 Mali 3
Guinea-Bissau 1 Zambia 1 
Tanzania 0 Egypt 2 
1730  Sierra Leone  Vs Sudan     
South Sudan 0 Mali 3
1800  Gambia Vs South Africa    
1830  Ivory Coast Vs Gabon       
1900 Sao Tome And Principe Vs Cape Verde    
Jumapili Juni 5
1530  Madagascar Vs Congo, DR
1600  Lesotho Vs Ethiopia
1600  Zimbabwe Vs Malawi        
1600  Swaziland Vs Guinea         
1600  Kenya Vs Congo     
1600  Central African Republic Vs Angola       
1600  Comoros Vs Burkina Faso  
1600  Mauritius Vs Ghana 
 1700 Benin Vs Equatorial Guinea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMA BIBLIA TAKATIFU HAPA

                                                        BONYEZA HAPA KUSOMA BIBLIA       

AZAM ACADEMY MABINGWA MICHUANO YA AFRIKA MASHARIKI

TIMU ya vijana ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC ‘Azam FC Academy’, usiku wa leo imefanikiwa kuwa mabingwa wa michuano ya vijana ya Afrika Mashariki ‘Azam Youth Cup 2016’ baada ya kuichapa Ligi Ndogo Academy kutoka Kenya mabao 3-0, mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex. Azam Academy inatwaa ubingwa huo ikiwa imefikisha jumla ya pointi tisa baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza nyingine zikiwa dhidi ya Future Stars Academy kutoka Arusha (4-1) na Football for Good Academy ya Uganda (5-1). Kikosi kizima cha Azam Academy na viongozi wao wakiwa na Kombe lao Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba (kulia) akimkabidhi tuzo mchezaji Shaaban Iddi baada ya kuibuka mfungaji bora Shujaa wa mabingwa hao kwenye mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wake hatari Shaaban Idd aliyepachika wavuni mabao mawili kwa ustadi mkubwa dakika ya 15 na jingine 90, alilolifunga kwa staili ya ‘tik-tak’ huku bao jingine likifungwa na mshambuliaji mwingine hodari w...

MUHIMBILI YAFANYA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE TATIZO MFUMO WA HEWA NA NJIA YA MKOJO.

 Kutoka kulia ni Dk. Zaitun Bokhary  na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula LEO kwa kushirikiana na  Profesa Saber  M. Waheeb (kushoto) na wenzake kutoka Misri.  Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na  Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.  Profesa Saber  M. Waheeb (katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo hayo leo.   Grace Joel akiwa na watoto wake pacha, Eliudi Joel  (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa wakiwa wameungana na baadaye walifan...